Kings FM Radio

Kings FM Radio

Share

šŸ”»Tunagusa Kila nyanja unayotamani kuisikiašŸ‘‚89.5-Njombe šŸ”»www.kingsfm.co.tz Chaugingi Street:
Njombe, Tanzania. http://tunein.com/radio/Kings-FM-1043-s263641/

Chaguo La Watu: Kings FM Radio Inatangaza Kutoka Njombe Tanzania, Ikiwa Na Lengo La Kuiweka Jamii Katika Level Ya Usawa Katika Burudani, Elimu Na Maadili.

13/10/2026

DAMASI ALIKUWA NA ā€˜VITU VYAKE’ ANAVYOFANYA - NABII

Mlezi wa kiroho wa Leonora Sanga, mke wa marehemu Damas Julias Mgaya, Nabii Mathias Mlokozi, amefunguka kuhusu namna alivyoshiriki katika kushughulikia mgogoro wa ndoa ya wanandoa hao.

Nabii Mlokozi amesema mume aliamua kuondoka katika chumba alichokuwa akilala na mkewe, akidaiwa kuwa na "Vitu Vyake" binafsi aliyokuwa akiyafanya ndani ya nyumba hiyo, ambayo yalichangia uamuzi wake wa kujitenga na mkewe.

13/10/2026

DAMAS ALINYIMWA UNYUMBA KWASABABU HAJAOKOKA_______ - Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Njombe

Akizungumza na , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, amethibitisha kifo cha mwanaume aliyetambulika kwa jina la Damas Mgaya, mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Mtaa wa Kambarage, eneo la Majengo, Kata ya Njombe Mjini, aliyekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuhusishwa na mgogoro wa ndoa, ambapo marehemu anadaiwa kutofautiana na mkewe kuhusu masuala ya unyumba, kwa madai kuwa mkewe alikataa kushiriki naye tendo la ndoa kwa sababu hakuwa ameokoka.

13/10/2026

DAMAS AJINYONGA, CHANZO NI KUNYIMWA UNYUMBA_________

Mwanaume aliyetambulika kwa jina la Damas Mgaya, mwenye umri wa miaka 38 na mkazi wa Mtaa wa Kambarage, eneo la Majengo, Kata ya Njombe Mjini, amekutwa amefariki dunia katika tukio linalodaiwa kuwa la kujinyonga.

Kwa mujibu wa mashuhuda, marehemu alikuwa akikabiliwa na migogoro ya ndoa ikiwa kunyimwa unyumba kwa muda mrefu, ambayo inadaiwa kuwa huenda ilichangia kutokea kwa tukio hilo.

.

13/10/2026

USIMAMIZI BORA WA MIFUMO ITAEPUSHA UPIGAJI BIMA YA AFYA KWA WOTE_________

Dorah Kacheche () x Mfaume Pastory (.pastory)

13/10/2026

SERIKALI NA MKONO MREFU KUKOMBOA WANANCHI WAKE_________
X Mfaume Pastory

KingsDrive

Photos from Kings FM Radio's post 13/10/2026

Mkuu wa Wilaya ya Makete, Kissa Gwakisa Kasongwa amekabidhi vifaa kwa jumuiya zinazojihusisha na uhifadhi wa Bonde la Ziwa Nyasa na kuhamasisha ufugaji wa nyuki, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha shughuli za uhifadhi wa mazingira na kutoa elimu kwa jamii.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na smoker na mavazi maalumu ya kujikinga na nyuki, vitakavyowasaidia wanajumuiya kutekeleza shughuli zao za ufugaji wa nyuki kwa usalama zaidi.

Pia, amekabidhi pikipiki zitakazorahisisha usafiri wa wanajumuiya kutoka eneo moja kwenda jingine kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi, kushiriki mikutano ya vijiji na kutembelea miradi ya ufugaji wa nyuki.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mfamasia Rabson Mahenge, amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa hatua hiyo, akieleza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuongeza ufanisi wa jumuiya hizo katika kutekeleza majukumu yao ya uhifadhi wa mazingira na kuhamasisha ufugaji wa nyuki.

Mahenge amesisitiza kuwa ufugaji wa nyuki ni miongoni mwa shughuli zinazoweza kuchangia uhifadhi wa mazingira na kuongeza kipato cha wananchi, hivyo amewahimiza wanajumuiya kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuendeleza elimu kwa jamii.

Jumuiya zilizotajwa ni Jumaruju na Jumaruchi, ambazo zinashiriki katika juhudi za kulinda Bonde la Ziwa Nyasa na kuhamasisha ufugaji wa nyuki.

13/10/2026

KUNA WALIOSEMA BIMA YA AFYA KWA WOTE NI CHANGA LA MACHO_______ - Mfaume Pastory

Akizungumzia maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa (), kwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri nchini, lengo ni kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, huku akisisitiza udhibiti wa ubadhirifu na wizi wa fedha za umma katika mpango huo.

šŸŽ™ļø Sikiliza Kings FM Radio 89.5 MHz au kupitia mtandaoni kwa kutumia RadioBox na TuneIn, kwa jina la KingsFMRadio.

13/10/2026

Mtangazaji wa Kipindi cha Fire Beats hapa Kings FM, DJ Tay C () amesema Wasanii wa sasa hawatengenezi Ngoma zinazofanya vizuri yaani ā€˜Hit Song’ k**a zamani.

Tay C amesema tatizo hilo sio la Muziki wa Bongofleva pekee ila ni Duniani kote ni ngumu Msanii kutengeneza Hits.

Ameongeza kuwa kwa sasa nyimbo zinazofanya vizuri kwenye maeneo mengi ni za zamani zinazorudiwa na Akili Mnemba (AI).

Je, unakubaliana na DJ Tay C? Tuambie hapo chini kwenye uwanja wa Comment.

12/10/2026

UDHAIFU WA DIMBA NI PALE WANAPOKUWA HAWANA MPIRA________ - Joshua Masebo () Mchambuzi W Michezo

12/10/2026

HATUNDUKE ASINGETIKA YANGA ANGEFUNGWA TU_________ - Joshua Masebo ()

Want your business to be the top-listed Media Company in Njombe?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address


Magereza Road, Chaugingi Street
Njombe

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kings FM Radio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Njombe.